Uongozi wa Vijana, 2013-2015
Uchaguzi uliofanyika Dominika ya Epifania, tarehe 06/01/2013, katika ukumbi wa parokia ulidhihirisha ukomavu wa vijana wa Kisarawe, ambapo waliwachagua viongozi wao kwa miaka mitatu ijayo. Hata kama viongozi watatu kati ya watano waliochaguliwa walishakuwa katika kamati Tendaji, walishika nafasi tofauti. Aliyekuwa Katibu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya naye alikuwa Mwenyekuwa akachukua nafasi ya Katibu. Aliyekuwa Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Mhazini mpya. Makamu Mwenyekiti na Katibu Msaidizi ni wapya katika kamati hii. Tunawapongeza Vijana wa Parokia hii kwa kuchagua viongozi wanaoaminika. Tuwaombee Vijana waendeleze ushirikiano huu na kuimarisha zaidi na zaidi utume kwa vijana. Tunawashukuru na kuwapongeza viongozi wapya kwa kukubali kuchukua uongozi na kuuendeleza ...