TYCS - Muungano wa Mt. Cottolengo (MOCK)
(TYCS – Minaki, Overland,
Chanzige, na Kimani)
s.l.p. 28017 kisarawe - pwani
1. Jina
Jina rasmi la Muungano Muungano wa Mt. Joseph Benedict
Cottolengo. Kifupi cha jina la Muungano ni Herufi za Kwanza za Matawi Husika. (MOCK – Minaki, Overland, Chanzige, na
Kimani).
2. Historia
TYCS
ni umoja wa wanafunzi wakatoliki Ulimwenguni. Inajulikana kama vijana wanafunzi
wakikristu. Hili kutimiza lengo la “kumleta Kristu katika mazingira ya
Mwanafunzi”, na kuwasaidia Vijana Wakatoliki kujiamini zaidi katika kuishi
maisha yao shuleni, ushirika huu wa kitume unaendelea kutafuta mbinu zaidi za
kuboresha mikakati yake. Moja ya mbinu hizo ni kuunda Kanda na Muungano, ambayo
huleta matawi zaidi pamoja hili kuwapa huduma za kiroho kwa urahisi na ufanisi.
Muungano
wa Mt. Joseph Benedict Cottolengo ulianzishwa mwaka 2010, ukileta pamoja matawi
ya Minaki Sekondari na Chanzige Sekondari, kwa wakati huo ukiitwa MICHA.
Wakitambua kwamba YCS ni njia nyoofu ya kuwasaidia vijana kuishi imani yao
vyema zaidi, Walezi na Viongozi wa matawi haya mawili, chini ya Ofisi ya Vijana
ya Parokia ya Mt. Stefano Shahidi, Kisarawe, waliweka misingi ya Muungano huu
kwa kuteua viongozi wa Kwanza wa Muda.
Mafanikio
mengi yalipatikana kwa kuwaleta pamoja vijana wa matawi haya mawili mara kwa
mara. Misa za Pamoja (Joint Mass), Kuwatembelea maskini (Matendo ya Huruma),
Kuunda kwaya ya Muungano wakishirikiana na Umoja wa Vijana Parokia, semina za
pamoja, na mafungo ni baadhi ya matukio yaliyodhihirisha mshikamano huo kuinua
ushiriki katika matawi husika.
Mwaka
2012, baada ya juhudi za kufungua matawi ya Sekondari za Kimani na Overland,
Viongozi wa Muungano pamoja na Walezi waliazimia kuupanua Muungano hili
kuyashirikisha Matawi hayo mawili. Ni katika zoezi la pamoja la Kuamua hatma ya
Muungano ambapo Viongozi wote na Walezi walikubaliana kubadilisha Muungano wa
Mt. Joseph Benedict Cottolengo (MICHA) kuwa MOCK.
Tarehe
26/05/2012 iliweka kuwa siku ya kuzindua Muungano huu wa MOCK. Katika shughuli
ile, Vijana wa Matawi ya Minaki, Chanzige na Kimani walishiriki kwa Wingi.
Walikuwa takriban 120, pamoja na baadhi ya walezi. Kaulimbiu ya siku ilikuwa,
“Kijana Mkatoliki na Imani”. Tawi la Overland alikuweza kushiriki kwa sababu ya
umbali.
Katika
tukio la pili la Muungano, matawi yote ya MOCK yalishiriki na hivyo kutimiza
ndoto za wanzilishi wa Muungano huu. Tarehe hiyo ya 30/09/2012, palikuwa na
Misa ya Pamoja, ambapo Kwaya ya Muungano iliongoza kwa nyimbo. Walezi wa matawi
yote walishiriki na vijana nao waliweza kukaa pamoja na kubadilishana mawazo.
3. Dhima
Lengo
kuu la Muungano wa Mt. Joseph Benedict Cottolengo ni kuwaleta vijana wakatoliki
pamoja katika urika unaowapa nafasi ya kukua pamoja na kuelimishana chini ya
walezi, kwa mfano wa Mt. Joseph Benedict Cottolengo.
4. Dhamira
Muungano
unatazamia kuwa Chachu ya maendeleo ya kiroho kwa vijana wa Sekondari zote (na
Vyuo) vya Kisarawe, kwa kuupeleka upendo wa Mungu Baba Mpaji kwa wahitaji wa
kila aina nje na ndani ya Muungano.
5. Tunu na Fadhila
Muungano
huu unaongozwa na tunu bora za maisha ya Kikristu alizofundisha Mt. Joseph
Benedict Cottolengo: Imani kwa Mungu Mpaji, Upendo kwa Maskini Ndugu zetu,
Matumaini makuu yaliyojengwa juu ya Upendo wa Mungu kwetu.
Vijana
wanajituma kuishi tangu sasa fadhila zote alizoishi kwa njia ya pekee Mt.
Joseph Benedict Cottolengo, yaani, Upendo wa dhati haswa kwa maskini, uadilifu,
bidii katika maisha, utulivu, furaha, na uchaji.
6. Kaulimbiu
Kaulimbiu
ya Muungano ni “Upendo wa Kristu unatumiliki” – Caritas Christi Urget Nos! (2 Kor 5:14).
7. Nembo
Alama
yetu ya wazi vijana walikusanyika chini ya Msalaba, ikiashiria kwamba Vijana
wanatambua Msalaba kama alama ya Ukombozi, kuitetea bila aibu, na kuishi
kulingana na mafundisho ya kanisa. Nembo hii inaweza kubadilishwa au kuongezwa
vipengele vinavyoonyesha lengo kuu la Muungano.
8. Uanachama
Kama
chama cha Wakristu wakatoliki kinachowaleta vijana pamoja kwa nia ya kuchangia
katika malezi yao ya kiroho, kijamii, kiakili, na kibinadamu, mwanachama lazima
atimize vigezo vifuatavyo:
1.
Awe Mwanachama hai wa
mojawapo wa Matawi yanayounda Muungano wa Mt. Joseph Benedict Cottolengo.
2.
Atimize vigezo
vilivyowekwa kwa uanachama wa TYCS, kulingana na Mwongozo wa YCS.
3.
Atimize vigezo
vinginevyo vinavyowekwa kupitia vikao halali vya Muungano vilivyoidhinishwa na
Walezi.
9. Uongozi
Tunatambua uongozi kama karama tunayopewa na
Mungu na hivyo viongozi wetu ni chachu ya kujituma katika kila jambo jema.
Muundo wa Uongozi ni ule ulioidhinishwa na TYCS kitaifa. Kwa kipengele hili,
tunatumia “Kitabu cha Kujiongoza.”
10. Itimisho
Somo wetu Mt. Joseph Benedict Cottolengo awe mfano na
mwombezi katika kutimiza. Alipokea ujumbe wa Kristu: “Tafuteni Kwanza Ufalme wa
Mbinguni na mengine yote mtayapata kwa ziada.” (Mt. 6:33). Lengo letu basi liwe
kutanguliza Ufalme wa Mbinguni hili mengine yote yawe Baraka kwetu.
Comments
Post a Comment
Thank you for visiting Bits of the Gospel. We appreciate your comments and support.