Tutafakari Maisha yake

Hand drawing-St. J B Cottolengo by Kirimo "Kwani wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu, kwa maana hamkupata roho ya utumwa mwogope tena, bali mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana wa Mungu na kuita, "Abba! Baba!" Roho mwenyewe hushuhudia roho zetu ya kuwa sisi ni wana, tu warithi pia, yaani warithi wa Mungu wanaorithi pamoja na Kristo, tukiwa tunavumilia mateso pamoja na Kristu, tupate kutukuzwa pamoja naye." (Rom. 8:14-17) Ni dhahiri kabisa kwamba Mt. Joseph Benedict Cottolengo sio tu mwana wa Mungu bali mwana Mpendwa na Mpenda Mungu. Upendo huu wa pekee kwa Mungu ulitokana na imani yake dhabiti. Kama Kijana alielimika katika mafundisho makuu ya imani. Alijua kuwa Mungu ametupa wote upendeleo wa pekee sana, ambapo kila mmoja wetu alipewa nafasi ya pekee machoni pa Mungu. Kwanza kabisa, imani hii ilimjengea msimamo na tabia ya aina yake. Katika utendaji kazi wake kama padre, alijitahidi kuwa na upendo wa pekee kwa kila mmoja, akiwapa nafasi ya...