Uchaguzi uliofanyika Dominika ya Epifania, tarehe 06/01/2013, katika ukumbi wa parokia ulidhihirisha ukomavu wa vijana wa Kisarawe, ambapo waliwachagua viongozi wao kwa miaka mitatu ijayo.
Hata kama viongozi watatu kati ya watano waliochaguliwa walishakuwa katika kamati Tendaji, walishika nafasi tofauti. Aliyekuwa Katibu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya naye alikuwa Mwenyekuwa akachukua nafasi ya Katibu. Aliyekuwa Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Mhazini mpya. Makamu Mwenyekiti na Katibu Msaidizi ni wapya katika kamati hii.
Tunawapongeza Vijana wa Parokia hii kwa kuchagua viongozi wanaoaminika. Tuwaombee Vijana waendeleze ushirikiano huu na kuimarisha zaidi na zaidi utume kwa vijana. Tunawashukuru na kuwapongeza viongozi wapya kwa kukubali kuchukua uongozi na kuuendeleza kulingana na mapokeo ya Kanisa Katoliki.
Mwaka huu wa Imani, uwe nafasi kwetu kuishi kikamilifu wito wetu kama Vijana wakatoliki.
Umoja wa Vijana
Parokia ya Mt. Stefano Shahidi Kisarawe
Viongozi wa Vijana
Mwenyekiti: Nd. Veronica Kavishe
M/Mwenyekiti: Nd. Matthias Kazonda
Katibu: Nd. Gernana Mchilla
Katibu Msaidizi: Nd. Stanley Haron
Mhazini: Nd. Alphonse Majugana
Walezi:
Sr. Maria Cesaria
Sr. Hellen Murungi
Fr. Nicholas Kirimo
mwenyezi mungu atutangulie katika kuhubiri na kuitangaza injili , umoja na ushirikiano miongoni mwetu ndio kiongozai mkubwa aliye juu yetu.
ReplyDelete