Posts

Showing posts from March, 2017

Appeal: The Marian Shrine of Mhaga, Kisarawe

Image
Kanisa la Mt. Bikira Maria Mama wa Miujiza ni Kituo cha Hija na Kituo cha Kiroho! Mwaka 2017, Kituo hiki kinalenga kuimarisha mazingira ya "Bustani ya Mama Maria" kwa kupanda miti, maua na kuweka uzio. Tunahitaji Kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini (20,000,000/=Tsh au 9500 USD) kukamilisha shughuli hii. The Church of the Blessed Virgin Mary Mother of the Miracles is a Shrine and a Spiritual Centre. This year 2017, the Shrine aims at improving the environment of "The Garden of Mother Mary" by planting trees, flowers and erecting a fence for security. We need around twenty million Shillings (20,000,000/= or 9500USD) to complete this phase of the project. You may participate in showing love to Mother Mary through a small donation: Account Name: COTTOLENGO TRUST TANZANIA BANK: EQUITY BANK TZ – QUALITY BRANCH, DAR ES SALAAM Account Number: 3001211140239 (Euro) or 3001211140240 (Tzs) SWIFT CODE: EQBLTZ  For more information contact us through:

Jubilee ya Miaka 100 ya Upadre Tanzania

Image
Jubilee ya Miaka 100 ya Upadre Tanzania   SALA YA KUWAOMBEA MAPADRE E e Bwana Yesu Kristu. Mkombozi wetu, kwa mapendo na tamaa yako ya kutaka kulinda vema Kanisa lako, ukachagua Mapadri wawe Wachungaji na Viongozi wa roho za watu. Nakuomba sana; ubariki nia na bidii inayowapasa Mapadri wote katika kazi zao. Uwaongezee Utakatifu. Uwatie moyo mzuri wenye mapendo makubwa kwako na roho za watu. Hivyo wakiisha kupata wenyewe Utakatifu, waweze kuwaongoza vizuri watu walio chini ya ulinzi wao, katika njia ya Utakatifu na furaha ya milele. Uwajalie neema zote za hali ya Upadri. Uwajalie ili waonyeshe kila siku ya maisha yao mfano wa kila fadhila ya mapendo na ya uaminifu katika Kanisa, kwa Baba Mtakatifu na kwa Maaskofu. Yesu mpendelevu, uangalie kwa mapendo kazi na mateso ya Mapadri wako; ubariki na ustawishe mafundisho yao; wanapowafundisha watoto, wanapowahubiria watu, wanapowatuliza wakosefu watubu na wanapowasaidia wagonjwa na wale wanaokaribia mauti, Ee Yesu uwe pamoj

Mhaga: Kwaresima ya Ukarimu

Image
Njia tano za Kuishi Kwaresima hii kwa Ukarimu Utangulizi Wapendwa Mahujaji, katika kipindi cha kwaresima, Baba Mtakatifu huwa anatuandikia barua yenye ujumbe maalum kwa ajili ya mfungo wetu. Umuhimu wa funga yetu unaonekana kabisa hata kwa kupitia barua hii. Tunaweza, basi kundonoa mambo baadhi ya kutuongoza katika kuifanya kwaresima yetu iwe karimu kweli. Sali zaidi, Funga kwa hiari, na Toa Zaidi “Kwaresima ni musimu wa kuzama zaidi katika maisha yetu ya kiroho kwa njia ya kutakatifuzwa inayotolewa na Kanisa: Kufunga,Kusali na kutoa sadaka.” Sala, kufunga na kutoa sadaka ni nguzo muhimu katika kukuza imani yetu na katika kuendeleza ukarimu wetu. Mambo ya kawaida kabisa kama kuacha kula nyama, tafakari ya kila siku na nafasi ya kutoa/kuwapa wengine vinapewa umuhimu na KristoYesu mwenyewe (Mt. 6:1-18, 25:31-40). Sali zaidi. Funga kwa hiari yako mwenyewe. Toa zaidi katika kanisa na kwa maskini jirani zako. Jiweke Huru “Badala ya kuwa chombo cha kutusaidia

Mhaga: Lolote atakalowaambieni, Fanyeni!

Image
Lolote atakalowaambieni, fanyeni! (2:1-12) Utangulizi Biblia ni barua ya Mungu. Kwa kuisoma tunamjua, tunaungana naye na kujipatia mwanga wa maisha yetu. Aidha, tunapata hisia chanya takatifu: tunahisi kupendwa, kusamehewa na kusaidiwa naye. Tukisoma na kulitafakari neno kwa makini tunatambua kuwa jambo alilomfanyia mwafulani/Israeli katika Biblia Mungu yu tayari kutufanyia kama hilo. Yesu, Maria na Kanisa Lake Katika harusi ya Kana ya Galilaya—Mama Maria yupo. Lakini na Yesu na wanafunzi wake walialikwa. Hapo, ishara ya kwanza itatendeka kwa ombezi la Mama Maria. Lakini tujiulize maswali matatu: a)       Mbona wanaharusi watindikiwe divai? Ina maana gani? b)       Mbona ni Maria tu anayetambua hilo hitaji? Bila kuombwa tena. c)       Bila Yesu na Maria ingekuwaje harusi ya Kana? Maria ni Jicho la Mungu Kwanza, kulingana na mapokea Maria alijiimarisha sana katika upendo wa jirani. Labda umaarifu wake unatokana na kuwa Mama wa “Mwalimu Yesu”. Lakini mbona “Msema

Mhaga: Kijiji cha Miujiza

Image
UTANGULIZI Kwa mgeni anayefika Parokia ya Kisarawe kwa mara ya kwanza, unaweza kufikiria ni parokia yenye mpangilio kama nyingine. Baada ya kugundua kuwa parokia hii ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam ina vigango zaidi ya 12, na kwamba kigango cha karibu zaidi kipo kilometa 13 na cha mbali zaidi kilometa 93, hapo utaelewa miundombinu na taratibu hapa ni tofauti na parokia nyingine. Mwaka huu 2017, Parokia ya Mt. Stefano Shahidi Kisarawe inatimiza miaka 17. Ilizinduliwa mwaka 1999 kuelekea Jubilei ya Mwaka 2000. Katika kuandaa mazingira kwa ajili ya uinjilishaji wa kwanza/msingi, pana umuhimu wa kuanzisha Jumuiya ndogondogo na Vigango. Kila mwaka vijiji ambavyo havina vigango karibu uomba kufunguliwa JNNK. Huo ndio msingi wa vigango vyenyewe. Jumuiya zinapokomaa na kufunguliwa nyingine, panakuwa na ulazima wa kufungua vigango.  Tuchukue mfano wa Kigango cha Bikira Maria Mama wa Miujiza, Mhaga. Kwa miaka mingi, ukanda huu wa Pwani hapakuwa kabisa na makanisa katika v