Kama unajua...

Kama unajua...

Utangulizi
Mara kwa mara katika malezi ya watoto na vijana, wazazi na walezi ulalamika sana wakisema vijana wao hawataki kutii tena. Kwa upande wao, watoto na vijana (hasa vijana), wanalalamika kwamba wazazi wao hawawaelewi na wanawanyima uhuru wao. Ukihoji vijana uhuru ni nini, mara nyingi wanajidai kueleza uhuru kuwa ni "nafasi ya kufanya kila mmoja atakavyo!" Na wazazi na walezi kwa pamoja wanapingana na mtazamo huu.

Bila shaka, kutaka kutenda bila kujali matokeo yake ni ujinga. Ni kama boti kuacha usukumwe na upepo bila mwelekeo. Inahitaji mwelekezi!
Uhuru ni nini?

Hekima za milenia za Kanisa Katoliki
Jibu la swali hili lipo katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki (KKK. 1731).
"Uhuru ni nguvu ndani ya mtu ya kukua na kukomaa katika ukweli na wema. Uhuru upata ukamilifu wake unapoelekezwa kwa Mungu, heri yetu."
Mizizi ya uhuru ipo katika akili na utashi. Hivyo, ni uwezo wa kutenda au kutotenda, kufanya hiki au kile, kutenda matendo yake mwenyewe na makusudi. Kwa njia ya utashi huru kila mtu anajiunda mwenyewe. Wewe ni fundi wa maisha yako mwenyewe. Utashi huru na akili ndivyo vitendeakazi vyako.

Hivyo, mvutano kati ya vijana na walezi wao unaweza kupunguzwa makali yake kwa wote (yaani vijana na walezi wenyewe) kupata malezi kuhusu uhuru. Kwa mfano, ni jambo jema kweli kuacha kufanya kazi zinazoendana na majukumu yako hili uambatane na rafiki yako "kula bata" wakati unapopaswa kuwa kazini? Lazima vijana wazoezwe kutambua majukumu yao mapema, nyumbani, shuleni, kanisani na katika jamii kwa ujumla. Hivyo, kila mmoja anaweza kujiuliza maswali yanayohusu lipi la kwanza, epi zake au kutimiza wajibu kwa Mungu na kwa jamii? Uwajibikaji sio kitu automatiki. Ni fadhila, ambayo inapatikana kwa zoezi la kutaka kuwajibika kila siku.

Kama unajua, basi wajuze na wengine! Au sio?

Comments

Post a Comment

Thank you for visiting Bits of the Gospel. We appreciate your comments and support.

Popular posts from this blog

TYCS - Muungano wa Mt. Cottolengo (MOCK)

Mwana Mpotevu au Waana Wapotevu?