Je, Unajua?

Je, unajua?

Katika kusafiri, mara kwa mara unasikia watu wakiongea kuhusu maswala ya imani katika daladala. Wanabishana na kugombana kuhusu mambo ambayo wanadhani ni muhimu kuyasimamia hata kwa "hasira".

Hivi, umeshajiuliza kama kuingia katika uzima wa milele (mbinguni) ni matokeo ya nini? Mimi nimejiuliza mara nyingi tu baada ya kumsikia bwana mmoja akimkemea mwenzake hadharani (katika mabasi ya kwenda mikoani), kwamba asipojituma zaidi katika "kumfurahisha Mungu" ataenenda zake jehanamu ya moto!

Busara za Mafundisho ya Kanisa Katoliki
Jibu lipo katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki:

"Heri ya uzima wa milele ni paji la Mungu tu; ni paji la kimungu kama ilivyo neema inayoelekeza huko." (KKK. 1726) Neema ni kipaji cha Mungu tunachopewa ili tuweze kufika mbinguni! Basi, kumbe kuingia mbinguni ni kwa neema tu. Hata kujituma hili uingie mbinguni ni swala la neema tu.

kazi ipo hapa: katika kutambua umuhimu wa neema hiyo kutoka kwa Mungu, kuiomba, kuitambua unapoipata, na kuishi kwa shukrani na unyenyekevu mkubwa zawadi hiyo ya pekee! Kumbuka neema ipo, kama inavyokuwa mikondo ya maji chini ya ardhi. Unahitaji utaalamu wa kuitambua mikondo hiyo na nguvu ya nia ya kutaka kuyachimba hayo maji.

Unajua sasa. Au sio?

Comments

Popular posts from this blog

TYCS - Muungano wa Mt. Cottolengo (MOCK)

Mwana Mpotevu au Waana Wapotevu?