TYCS Kanda ya Mt. Aloyce - Pugu


RIPOTI YA MAAFALI YA KIDATO CHA SITA

KANDA YA MT. ALOYCE – PUGU

 

UTANGULIZI

Maafali ni sherehe ya kuwaaga na kuwapongeza ndugu wanaovuka hatua moja na kuelekea nyingine katika masomo. Mnamo tarehe 19/01/2013, kulikuwa na maafali ya kidato cha VI yaliyofanyika katika viwanja vya Parokia ya Kisarawe. Maafali haya ni shere ambayo hujumuisha na kushirikisha shule mbalimbali za sekondari katika Kanda ya Mt. Aloyce – Pugu.

Mahafali ya mwaka huu yalikuwa ya pekee mno, kwani yalipata kuwa na washiriki wengi kutoka sehemu tofauti tofauti katika kanda yetu. Pia yalifanyika kwa mara ya Kwanza katika Parokia ya Kisarawe, kinyume na miaka ya nyuma.

LENGO

Maafali haya yalikuwa na malengo kama yafuatayo:

Ã…      Kumshukuru Mungu pamoja na wahitimu kwa kuwafikisha hapo walipofikia salama yaani kidato cha sita.

Ã…      Wahitimu kuomba msaada kwa Mungu ili waweze kuongozwa na Roho wake katika kipindi hiki cha mwisho wa masomo yao ya sekondari.

Ã…      Kupata fursa ya uinjilishaji rika kati ya wanaTYCS.

Ã…      Kuwapongeza na kuwatunuku vyeti wahitimu.

Ã…      Kupata nasaha za kimalezi kutoka kwa Mgeni Rasmi na walezi.

Malengo haya yote yalitimia kwa kiasi kikubwa na kwamba kila kitu kilienda kulingana na mpango.

MAANDALIZI

Maandalizi ya maafali haya yalifanyika chini ya uongozi wa Kanda kwa ushirikiano mkubwa wa Mlezi wa Vijana Parokia ya Kisarawe Pd. Kirimo, mwalimu mlezi kanda, Katibu wa Vijana Jimbo, na matawi yaliyopo katika kanda hii.

Vilifanyika vikao sita (6), Minaki, Pugu, na Parokiani Kisarawe. Vikao hivi viliwakutanisha viongozi wa Kanda na Fr. Kirimo, Mwalimu mlezi wa kanda, wawakilishi wa Kidato cha Sita, na Viongozi mbalimbali wa Matawi ya kanda. Agenda zilikuwa kama ifuatavyo:

Ã…      Ukusanyaji wa Fedha

Ã…      Kuwafikia wahitimu wa Matawi mbalimbali

Ã…      Orodha ya mahitaji ya maafali

Ã…      Mapendekezo ya Kidato cha Sita

Ã…      Mgeni Rasmi

Ã…      Ratiba

Ã…      Bajeti na Mengineyo.

Ili kuwa na mgawanyo mzuri wa majukumu kamati mbalimbali ziliundwa kama ifuatavyo:

1.    Mipango na Manunuzi

2.    Jenga TYCS – Kanda

3.    Chakula na Vinywaji

4.    Mapokezi na Ulinzi

5.    Afya na Usafi wa Mazingira

6.    Liturjia

7.    Burudani (Musiki & S. System)

8.    M.C.

Wana TYCS walionyesha moyo wa kujitolea kwani walishiriki kwa uchangamfu na uangalifu katika kamati walizopangiwa.

USHIRIKI WA WANATYCS

Fomu na kadi maalum ziliandaliwa ili kuwezesha maafali haya. Fomu hizi na kadi ziligawiwa kwenye matawi ya kanda na katika Parokia ya Pugu na Kisarawe.

Maafali yalishirikisha shule kumi (10) zilizopo chini ya Kanda ya Mt. Aloyce-Pugu. Jedwali lifuatalo linaonyesha ushiriki huo.

 
SHULE/TAWI
IDADI
WALEZI
MICHANGO
1.
MINAKI
91
-
643000
2.
PUGU
60
2
387000
3.
OVERLAND
47
2
188500
4.
DR. DIDAS
25
1
80000
5.
HALISI
20
-
22000
6.
PUGU STATION
8
-
20000
7.
FURAHA
4
-
16000
8.
NGUVU MPYA
3
-
8000
9.
CHANZIGE
3
-
12000
10
KINYAMWEZI
2
-
6000
 
JUMLA
273
4
1376500

 

Maafali yalikuwa na wageni waalikwa zaidi ya 30. Vilevile yaliudhuliwa na Padre, Masista na Vijana wa Parokia za Kisarawe na Pugu.

Mgeni Rasmi katika maafali haya alikuwa Dr. Peter D. Kafumu. Aliwasisitiza wahitimu na wanafunzi wengine juu ya umuhimu wa kutambua wito wao mapema, vilevile alisisitiza kuwa na maadili mema hasa katika umri huu wa ujana. Kwa kuwa kanda ina upungufu wa fedha, mgeni rasmi aliahidi kuchangia mfuko wa Kanda shilingi laki nne (Tsh 400 000). Pia mgeni mwandamizi, Katibu wa Jimbo aliahidi shilingi tisini elfu (Tsh 90 000), kutunisha mfuko huu.

Mgeni Rasmi aligusia swala la imani kama la msingi sana. Aliwaonya vijana dhidi ya kuwekeza upande mmoja tu (wa masomo) huku wakisahau au kupuuzilia imani. “Mtumikie Mungu katika ujana wako!” alirudia maneno ya Biblia Takatifu.

BAJETI YA MAAFALI

Bajeti ya maafali iliandaliwa na Kamati Kuu. Imeambatanishwa katika ripoti hii.

 

KUFANIKIWA KWA MAAFALI

Maafali yalifanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri baina ya viongozi wa Kanda na matawi, Pd. Kirimo, Mwalimu mlezi wa Kanda, wanaTYCS, Masista na Vijana kutoka Parokia za Kisarawe na Pugu.

Maafali haya yaliwajenya vijana kiroho na kuwakomaza kiimani kutokana na mahubiri mazuri yalizokuwa na mada kuu uinjilishaji kwa njia ya mifano ya maisha, na nasaha za kuvutia kutoka kwa Mgeni Rasmi.

Kwa upande wa Liturujia, ushiriki wa vijana ulikuwa wa kutukuka kwani kwaya ya Muungano wa Mt. Cottolengo iliongoza kwa njia ya kusisimua. Vijana walionekana kufurahia na kuyapokea mahubiri, na zaidi walikuwa watulivu. Nidhamu ya hali ya juu ilishuhudiwa katika tukio hili. Vijana walionekana kuelewa umuhimu wa kutangamana kati yao bila kuzua vurugu au uvunjifu wa amani katika tukio hili. Hali ya usalama pia ilikuwa nzuri.

Kamati ya Chakula na vinywaji ilifanikisha shughuli ya ugawaji wa vyakula na vinywaji. Kila mshiriki alipata kula na kunywa, na ilionekana kwamba wengi walifurahia vyakula.

Shukrani za dhati kwa wote waliowezesha maafali haya. Mungu awabariki.

 

CHANGAMOTO

Tulikumbana na changamoto kadha wa kadha ambazo tulikabiliana nazo na tutaendelea kukabiliana nazo hili kuboresha hali ya Kanda hii.

Ã…      Kutoshiriki kwa baadhi ya Matawi yalioyomo chini ya Kanda hii.

Ã…      Kuzidi kwa idadi ya washiriki kadiri ya makadirio.

Ã…      Mabadiliko ya Mihula yaliyochangia katika kukwama kwa ukusanyaji wa Michango katika muda mwafaka.

Ã…      Kutofuata ratiba ya siku kutokana na kuchelewa kwa matawi yaliyo mbali na Kisarawe.

MAPENDEKEZO

Kamati Kuu ya Kanda na wanaTYCS walipendekeza yafuatayo:

Ã…      Kuwepo kwa Coupon/voucher za uhakika zaidi ili kuepuka tatizo la kugawa chakula na vinywaji.

Ã…      Kamati ndogondogo ziundwe mapema na zipewe orodha ya majukumu yao mapema.

Ã…      Kuwepo na tamasha, kongamano, na misa za pamoja ili kukuza imani na kuujenga umoja kati ya vijana wakatoliki.

HITIMISHO

Katika mwaka huu wa Imani, tukio la maafali ya Kanda yetu limekuwa kichocheo cha imani na ushiriki hai wa TYCS katika maisha ya Kanisa. Ni matumaini yetu kuwa kila tukio la Kanda yetu litachangia katika kukuza, kueneza, na kusherehekea imani yetu katoliki.

Tunamwomba Bwana, sisi tunaotamani kubaki katika uwepo wake, tuongezewe imani, mwaka huu wa imani na maisha yetu yote.


 

RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI
MAAFALI YA TYCS FORM 6 - KANDA YA MT. ALOICE PUGU
KISARAWE - 19/01/2013

 
 
 
 
 
 
 
 
MAPATO
 
 
MATUMIZI
 
 
1
VIWAWA
64000
1
CHAKULA
900000
 
2
JUMUIA
100000
2
MAJI & SODA
265100
 
3
UFADHILI
46000
3
S.SYSTEM
50000
 
4
MICHANGO 1
195000
4
KEKI
45000
 
5
MICHANGO 2
744500
5
VITI
40000
 
6
MICHANGO 3
56000
6
MAPAMBO
40000
 
7
MICHANGO 4
72000
7
ZAWADI M.R.
13500
 
8
MICHANGO 5
102000
8
TURUBAI
12500
 
9
MICHANGO 6
9000
9
USAFIRI -TURUBAI
8000
 
10
MICHANGO 7
24000
10
KAMBA
1500
 
11
MICHANGO 8
104000
11
SABUNI
1200
 
12
JUMLA KUU
1516500
12
PHOTOCOPY Counter BK
13500
 
 
 
 
13
STICKS &  balloons
1800
 
 
 
 
13
Mawasiliano
1000
 
 
 
 
15
Usafiri Vifaa & petrol generator
50000
 
 
 
 
 
JUMLA
1443100
 
 
 
 
16
SALIO
73400
 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

TYCS - Muungano wa Mt. Cottolengo (MOCK)

Mwana Mpotevu au Waana Wapotevu?