KONGAMANO LA VIJANA, MWAKA WA IMANI (PAROKIA YA KISARAWE)
KONGAMANO: OVERLAND HIGH SCHOOL, MARUMBO UTANGULIZI "Someni kwa bidii, jiwekeni daima karibu na Mungu, na mkuze fadhila za uchapakazi na uadilifu kuanzia umri huu mdogo. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu." Maneno hayo ya Mhashamu Askofu Titus Joseph Mdoe, ni nasaha iliyoliashiria kufikia kilele cha Kongamano la Vijana, Mwaka wa Imani lililoandaliwa na Ofisi ya Vijana, Parokia ya Kisarawe. Kuanzia tarehe 06/06/2013, Alhamisi Jioni hadi 09/06/2013 Jumapili Jioni, takriban vijana 180 walishiriki pamoja na walezi wao katika lililochukua kaulimbiu yake kutoka Injili ya Luka. Luka 17:5 " Bwana Tuongezee imani” . Katika kufanikisha lengo la Kongamano hili, walezi wa Vijana wakiongozwa na Pd. Kirimo walihamasisha na kusimamia...