Tendo la Huruma
Tafakari ya Matendo Saba ya Huruma ya Kiroho
Hivi, unajua kuwa Maandiko Matakatifu yanasherehekea sana Huruma ya Mungu? Angalia haya hapa:
"Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashikilii hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema." (Mik. 7:18)
Hamna manufaa kwake kushikilia hasira yake wala kuweka kumbukumbu ya dhambi za watu wake. badala yake, kwa moyo wa huruma kabisa, anawasamehe watu wake. Hatupati manufaa yoyote hata sisi tunaposhikilia na kuweka kumbukumbu ya maovu tuliyotendewa na wenzetu. Ni hasara tupu kuweka hasira, kinyongo na hisia za kutaka kulipiza kizazi. Na ndani ya mioyo ya wanadamu mna kila sababu ya watu kusameheana.
Pana manufaa kuwasamehe wakosefu! Katika sala ya Baba Yetu tayari huwa tunasema, "Utusamehe makosa yetu, kama sisi tuwasameheavyo waliotukosea!" Ni ombi lenye masharti ya kujiwekea. Unasamehe na unaomba msamaha!

Comments
Post a Comment
Thank you for visiting Bits of the Gospel. We appreciate your comments and support.