JE, UNAICHUKULIAJE BIBLIA?
Je, unaichukuliaje
Biblia?
Kwa maoni yako …
- ni tunda la busara
za mwanadamu?
- ni kitambu cha
hadithi na nahau?
- ni Neno la Mungu?
Biblia inasemaje?
“Maandiko matakatifu
yote ni uvuvio kutoka kwa Mungu.” (2 Timotheo 3:16)
Ina maana hii kwako:
- majibu ya kuridhisha
juu ya mambo makubwa ya maisha (Methali 2:15).
- misingi dhabiti ya
maisha ya kila siku (Zaburi 119:105).
- matumaini halisi ya maisha ya baadaye (Warumi 15:4)
TUNAWEZA KUAMINI
INACHOSEMA BIBLIA?
Ndio, angalau kwa
sababu tatu:
ü
Mwendelezo
wa ajabu
Biblia
imeandikwa ndani ya miaka 1600 na watu kama arobaini hivi. Wengi wao
hawajulikani kamwe.
ü
Uwazi
katika kueleza historia.
Wanahistoria
kawaida hujaribu kuficha kushindwa kwa watu wao. Baadala yake, waandishi wa
Biblia wanaripoti kila kitu bila kuficha mapungufu yao na ya taifa yao. (2
Nyakati 36:15, 16: Zaburi 51:1-14)
ü
Kutimia
kwa unabii
Biblia
ilitabiri kuanguka kwa mji wa Babilonia karibia miaka 200 kabla ya kutokea
kwake (Isaia 13:17-22). Ilieleza sio tu jinsi mji huu ungeanguka bali pia jina
la yule aliyeuteka (Isaia 45:1-3).
Mambo mengine mengi
yaliyoandikwa yametimia. Je, nasi tutarajie
nini kutoka kwa Mungu? (2 Petro 1:21)
Comments
Post a Comment
Thank you for visiting Bits of the Gospel. We appreciate your comments and support.