Kama unajua...
Kama unajua... Utangulizi Mara kwa mara katika malezi ya watoto na vijana, wazazi na walezi ulalamika sana wakisema vijana wao hawataki kutii tena. Kwa upande wao, watoto na vijana (hasa vijana), wanalalamika kwamba wazazi wao hawawaelewi na wanawanyima uhuru wao. Ukihoji vijana uhuru ni nini, mara nyingi wanajidai kueleza uhuru kuwa ni "nafasi ya kufanya kila mmoja atakavyo!" Na wazazi na walezi kwa pamoja wanapingana na mtazamo huu. Bila shaka, kutaka kutenda bila kujali matokeo yake ni ujinga. Ni kama boti kuacha usukumwe na upepo bila mwelekeo. Inahitaji mwelekezi! Uhuru ni nini? Hekima za milenia za Kanisa Katoliki Jibu la swali hili lipo katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki (KKK. 1731). "Uhuru ni nguvu ndani ya mtu ya kukua na kukomaa katika ukweli na wema. Uhuru upata ukamilifu wake unapoelekezwa kwa Mungu, heri yetu." Mizizi ya uhuru ipo katika akili na utashi. Hivyo, ni uwezo wa kutenda au kutotenda, kufanya hiki au kile, kutenda matendo yake mwe...