Kanda ya Mt. Aloyce, Pugu: Tawi la Kimani
Ufunguzi wa Tawi la Kimani Secondary School – Kisarawe Kanda ya Mt. Aloyce – Pugu Friday, May 10, 2013 _____________________________________________________ Utangulizi Kwa mkusanyiko huu wa watu, kwa maandalizi haya ya kipekee kabisa, kwa Ibada hii ya Misa Takatifu, tunazindua rasmi tawi la TYCS Kimani, Kanda ya Mt. Aloyce Pugu. Ni tendo la imani. Na kwetu vijana wakatoliki, ikizingatiwa kuwa huu ni Mwaka wa Imani, sina shaka kabisa tendo hili linatuimarisha zaidi kiroho. Kama TYCS ni chama cha Kitume kinachowaleta pamoja Vijana Wakatoliki wa Shule za sekondari hili kumleta Kristo katika mazingira ya shule, ni wazi kabisa kwamba leo, kwa njia ya Pekee, Kristo anakuja katika mazingira ya shule ya Kimani (Wilaya ya Kisarawe). Yesu anakuja sio kuingilia programu za shule au kuvuruga amani yetu kama wanafunzi bali kut...