Mwana Mpotevu au Waana Wapotevu?
Injili ya Kwaresima: Utangulizi Nafikiri sio rahisi sana kutoa tafakari kuhusu Mwana Mpotevu. Inaitwa pia Injili ya Baba mwenye huruma. Tutagundua kuwa ina majina zaidi ya haya leo. Mojawapo ya vipengele vinavyovutia zaidi vya Maisha ya Kiroho (mafundisho) ya Mt. Joseph Cottolengo ni msisitizo anaweka katika “Kuwa katika uhusiano mwema na Mungu”. Alitaka ziive kati ya wafuasi wake na Mungu. Na Injili hii (Luka 15:11-32) inatusaidia kutathmini kama tupo sawa. Labda inafaa kufikiria ni wana wawili wapotevu. Hebu tuitafakari pamoja kama Walezi wa Watoto Wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu. Kupotelewa na Mwana! Huzuni. Niaminini kweli. Unaweza kuvumilia mara mia kupotelewa na kondoo au hata hela (haya 1-10) kuliko kuvumilia kupotelewa na mtoto. Injili hii utumika mara nyingi kama maandalizi ya maungamo. Inaonyesha picha ya Baba asiyekata tamaa, mwenye huruma kubwa. Hisia tunazopata kuhusiana na tabia ya huyu kijana aliyepotea, na kule kurudi kwake...