Posts

Showing posts from June, 2013

KONGAMANO LA VIJANA, MWAKA WA IMANI (PAROKIA YA KISARAWE)

Image
KONGAMANO: OVERLAND HIGH SCHOOL, MARUMBO UTANGULIZI "Someni kwa bidii, jiwekeni daima karibu na Mungu, na mkuze fadhila za uchapakazi na uadilifu kuanzia umri huu mdogo. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu." Maneno hayo ya Mhashamu Askofu Titus Joseph Mdoe, ni nasaha iliyoliashiria kufikia kilele cha Kongamano la Vijana, Mwaka wa Imani lililoandaliwa na Ofisi ya Vijana, Parokia ya Kisarawe. Kuanzia tarehe 06/06/2013, Alhamisi Jioni hadi 09/06/2013 Jumapili Jioni, takriban vijana 180 walishiriki pamoja na walezi wao katika lililochukua kaulimbiu yake kutoka Injili ya  Luka.                                                                     Luka 17:5 " Bwana  Tuongezee imani” . Katika kufanikisha lengo la Kongamano hili, walezi wa Vijana wakiongozwa na Pd. Kirimo walihamasisha na  kusimamia maandalizi yaliyochukua zaidi ya mwezi mzima. Mada Kadha wa kadha zilitolewa ikiwemo Kujikuza katika Imani (Nd. Silvanus M.), Utunzaji na uwekezaji katika Mazingira (Mwelimi